Matunda ya wenye haki na wapenda amani

Bible reading Swahili

Nukuu kutoka kwa Neno la Mungu.

“17 Lakini hekima itokayo juu mbinguni, kwanza ni safi; inapenda amani, upole na huwajali watu; imejaa huruma na huzaa matunda ya matendo mema; haina ubaguzi wala unafiki. 18 Uadilifu ni mazao ya mbegu ambazo wapenda amani hupanda katika amani.” (James 3:17-18 Swahili)

“Kuadhibiwa si jambo la kufurahisha bali la kuhuzunisha. Lakini wale waliofunzwa kuwa na nidhamu mwishowe watavuna tuzo la amani kutoka katika maisha adili!” (Hebrews 12:11 Swahili)

18 aMtu mwovu hupata ujira wa udanganyifu,
bali yeye apandaye haki huvuna tuzo ya uhakika.
” (Proverbs 11:18 Swahili)

17 aMatunda ya haki yatakuwa amani,
matokeo ya haki yatakuwa utulivu
na matumaini milele.
” (Isaiah 32:17 Swahili)

“22 Lakini matokeo ya kuongozwa na Roho ni mapendo, furaha, amani, uvumilivu, wema, fadhili, uaminifu, 23 upole na kuwa na kiasi. Hakuna Sheria inayoweza kupinga mambo hayo.” (Galatians 5:22-23 Swahili)

12 aJipandieni wenyewe haki,
vuneni matunda ya upendo usio na kikomo,
vunjeni ardhi yenu isiyolimwa;
kwa kuwa ni wakati wa kumtafuta Bwana,
mpaka atakapokuja
na kuwanyeshea juu yenu haki.
” (Hosea 10:12 Swahili)

“Apandaye katika tamaa za kidunia, atavuna humo uharibifu; lakini akipanda katika Roho, atavuna kutoka kwa Roho uzima wa milele.” (Galatians 6:8 Swahili)

“Maana Utawala wa Mungu si shauri la kula na kunywa, bali unahusika na kuwa na uadilifu, amani na furaha iletwayo na Roho Mtakatifu.” (Romans 14:17 Swahili)

“Basi, tangu sasa, sisi hatumpimi mtu yeyote kibinadamu. Hata kama kwa wakati mmoja tulimpima Kristo kibinadamu, sasa si hivyo tena.” (2 Corinthians 5:16 Swahili)

“Maisha yenu yatajazwa mambo yote yaliyo kweli bora, ambayo Yesu Kristo mwenyewe anaweza kuwajalieni, kwa ajili ya utukufu na sifa ya Mungu.” (Philippians 1:11 Swahili)


28 aYeyote ategemeaye utajiri wake ataanguka,
bali mwenye haki atastawi kama jani bichi.
” (Proverbs 11:28 Swahili)

30 aTunda la mwenye haki ni mti wa uzima,
naye mwenye hekima huvuta roho za watu.
” (Proverbs 11:30 Swahili)

“Heri wenye kuleta amani, maana wataitwa watoto wa Mungu.” (Matthew 5:9 Swahili)

“Mvunaji anapata mshahara wake, na anakusanya mavuno kwa ajili ya uzima wa milele; hivyo mpandaji na mvunaji watafurahi pamoja.” (John 4:36 Swahili)

“9  Sala yangu ni hii: naomba upendo wenu uzidi kuongezeka zaidi na zaidi pamoja na ujuzi wa kweli na busara ya kila namna, 10 ili mweze kuchagua jambo lililo bora. Hapo ndipo mtakuwa safi na bila lawama yoyote ile katika siku ile ya Kristo. 11 Maisha yenu yatajazwa mambo yote yaliyo kweli bora, ambayo Yesu Kristo mwenyewe anaweza kuwajalieni, kwa ajili ya utukufu na sifa ya Mungu.” (Philippians 1:9-11 Swahili)

“Furahini kuhusu jambo hilo, ijapokuwa sasa, kwa kitambo kidogo, itawabidi kuhuzunika kwa sababu ya majaribio mbalimbali mnayoteseka.” (1 Peter 1:6 Swahili)

“Na sasa imebakia tu kupewa tuzo la ushindi kwa maisha ya uadilifu, tuzo ambalo Bwana Hakimu wa haki, atanipa mimi Siku ile na wala si mimi tu, ila na wale wote wanaotazamia kwa upendo kutokea kwake.” (2 Timothy 4:8 Swahili)

+

Tazama pia maandishi yaliyotangulia

  1. Maandiko ya Biblia kuhusu upendo na amani yatakayoshirikiwa katika mkutano huo
  2. Mahali pa kukutania ili kushiriki amani na upendo wao k

Un commentaire sur « Matunda ya wenye haki na wapenda amani »

Laisser un commentaire