Maandiko ya Biblia katika: Kumiliki duniani katika wokovu wote


Vipande vya Biblia vya ziada kwa: Mali duniani katika wokovu wote

Quotes from God’s Word.

“Nimekufanya ujulikane kwao na nitaendelea kufanya hivyo, ili upendo ulio nao kwangu uwe ndani yao, nami niwe ndani yao. »” (Joh 17:26 Swahili)“Ikiwa basi Mungu hulivika hivyo jani la shambani ambalo leo liko na kesho latupwa motoni, je, hatafanya zaidi kwenu ninyi? Enyi watu wenye imani haba!” (Mt 6:30 Swahili)“Lakini, kama Mungu hulivika vizuri jani la shambani ambalo leo liko na kesho latupwa motoni, je, hatawafanyia ninyi zaidi? Enyi watu wenye imani haba!” (Lu 12:28 Swahili)

“Kwake yeye aliye Mfalme wa milele na asiyekufa, yeye aliye Mungu pekee—wake viwe heshima na utukufu milele na milele! Amina.” (1Ti 1:17 Swahili)

“akaapa kwa jina la Mungu aishiye milele na milele, Mungu aliyeumba mbingu na vyote vilivyomo, bahari na vyote vilivyomo, dunia na vyote vilivyomo. Akasema, « Wakati wa kusubiri zaidi umekwisha!” (Re 10:6 Swahili)

“Maana Mungu aliupenda ulimwengu hivi hata akamtoa Mwana wake wa pekee, ili kila amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” (Joh 3:16 Swahili)

“Hata hivyo, Mungu hakuacha kujidhihirisha kwa mambo mema anayowatendea: huwanyeshea mvua toka angani, huwapa mavuno kwa wakati wake, huwapa chakula na kuijaza mioyo yenu furaha. »” (Ac 14:17 Swahili)

“Yeye ni mng’ao wa utukufu wa Mungu, na mfano kamili wa hali ya Mungu mwenyewe, akiutegemeza ulimwengu kwa neno lake lenye nguvu. Baada ya kuwapatia binadamu msamaha wa dhambi zao, aliketi huko juu mbinguni, upande wa kulia wa Mungu Mkuu.” (Heb 1:3 Swahili)

“Saa ileile, Yesu akafurahi kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, akasema, « Nakushukuru ee Baba, Bwana wa mbingu na dunia, kwa kuwa umewaficha wenye hekima na elimu mambo haya, ukawafumbulia wadogo. Naam, Baba, ndivyo ilivyokupendeza. »” (Lu 10:21 Swahili)

“Ndiyo kusema, Mungu aliyachagua yale ambayo ulimwengu huyaona ni upumbavu, ili awaaibishe wenye hekima; na aliyachagua yale ambayo ulimwengu huyaona ni dhaifu, ili awaaibishe wenye nguvu.” (1Co 1:27 Swahili)

“Tangu Mungu alipoumba ulimwengu, uwezo wake wa milele na uungu wake, ingawa havionekani kwa macho, vinafahamika wazi. Watu wanaweza kuyajua mambo hayo kutokana na vitu hivyo alivyoumba Mungu. Kwa hiyo hawana njia yoyote ya kujitetea!” (Ro 1:20 Swahili)

“ili mpate kuwa watoto wa Baba yenu aliye mbinguni. Kwa maana yeye huwaangazia jua lake watu wabaya na wema, na kuwanyeshea mvua watu wanyofu na waovu.” (Mt 5:45 Swahili)

“Adamu wa kwanza aliumbwa kwa udongo, alitoka ardhini; mtu wa pili alitoka mbinguni.” (1Co 15:47 Swahili)

“ »Ndiyo maana nawaambieni, msiwe na wasiwasi juu ya chakula na kinywaji mnavyohitaji ili kuishi, wala juu ya mavazi mnayohitaji kwa ajili ya miili yenu. Je, maisha ni chakula tu au zaidi? Na mwili, je, si zaidi ya mavazi?” (Mt 6:25 Swahili)

“Heri wenye kuleta amani, maana wataitwa watoto wa Mungu.” (Mt 5:9 Swahili)

“ »Wewe ni Bwana na Mungu wetu, unastahili utukufu na heshima na nguvu; maana wewe uliumba vitu vyote, na kwa matakwa yako kila kitu kimepewa uhai na uzima. »” (Re 4:11 Swahili)

“Vivyo hivyo, ni lazima mwanga wenu uangaze mbele ya watu, ili wayaone matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni. »” (Mt 5:16 Swahili)

“Akasema kwa sauti kubwa, « Mcheni Mungu na kumtukuza! Maana saa imefika ya kutoa hukumu yake. Mwabuduni yeye aliyeumba mbingu na nchi, bahari na chemchemi za maji. »” (Re 14:7 Swahili)

“Nikasikia viumbe vyote mbinguni, duniani, chini kuzimuni na baharini—iumbe vyote ulimwenguni—ikisema: « Kwake yeye aketiye katika kiti cha enzi, na kwa Mwanakondoo, iwe sifa na heshima na utukufu na enzi milele na milele. »” (Re 5:13 Swahili)

“wakisema, « Amina! Sifa, utukufu, hekima, shukrani, heshima, uwezo na nguvu viwe kwa Mungu wetu, milele na milele! Amina! »” (Re 7:12 Swahili)

“wakisema: « Bwana Mungu Mwenye uwezo, uliyeko na uliyekuwako! Tunakushukuru, maana umetumia nguvu yako kuu ukaanza kutawala!” (Re 11:17 Swahili)

“Kisha nikasikia sauti kubwa kutoka mbinguni ikisema: « Sasa ukombozi utokao kwa Mungu umefika! Nguvu na Utawala wa Mungu wetu umedhihirika. Na Kristo wake ameonyesha mamlaka yake! Maana yule mdhalimu wa ndugu zetu, aliyesimama mbele ya Mungu akiwashtaki usiku na mchana, sasa ametupwa nje.” (Re 12:10 Swahili)

“tena niwaangazie watu wote waone jinsi mpango wa Mungu uliofichika unavyotekelezwa. Mungu aliye Muumba wa vitu vyote alificha siri hiyo yake tangu milele,” (Eph 3:9 Swahili)

“Mkaribieni Mungu, naye atakuja karibu nanyi. Osheni mikono yenu enyi wakosefu! Safisheni mioyo yenu enyi wanafiki!” (Jas 4:8 Swahili)

“Maana hawakufahamu jinsi Mungu anavyowafanya watu wawe waadilifu, na wamejaribu kuanzisha mtindo wao wenyewe, na hivyo hawakuikubali njia hiyo ya Mungu ya kuwafanya wawe waadilifu.” (Ro 10:3 Swahili)

“Zaidi ya hayo sisi tunawaheshimu wazazi wetu waliotuzaa hata wanapotuadhibu. Basi, tunapaswa kumtii zaidi Baba yetu wa kiroho ili tupate kuishi.” (Heb 12:9 Swahili)

“Waheshimuni watu wote, wapendeni ndugu zenu waumini, mcheni Mungu, mheshimuni mfalme.” (1Pe 2:17 Swahili)