“Tusiache ile desturi ya kukutana pamoja, kama vile wengine wanavyofanya. Bali tunapaswa kusaidiana kwani, kama mwonavyo, Siku ile ya Bwana inakaribia.” (Hebrews 10:25 Swahili)
“Kwa maana popote pale wanapokusanyika wawili au watatu kwa jina langu, mimi nipo hapo kati yao. »” (Matthew 18:20 Swahili)
“Hawa wote waliendelea kujifunza kutoka kwa mitume, kuishi pamoja kidugu, kumega mkate na kusali.” (Acts 2:42 Swahili)
“Huwaongoza wanyenyekevu katika haki,
naye huwafundisha njia yake.” (Psalms 25:9 Swahili)
“Ingawa Bwana yuko juu,
humwangalia mnyonge,
bali mwenye kiburi
yeye anamjua kutokea mbali.” (Psalms 138:6 Swahili)
“Mtu mwenye haki na anipige: ni jambo la huruma;
na anikemee: ni mafuta kichwani mwangu.
Kichwa changu hakitalikataa.
Hata hivyo, maombi yangu daima
ni kinyume cha watenda mabaya,” (Psalms 141:5 Swahili)
“Mimi ndiye mwenye kumwonya na kumrudi yeyote ninayempenda. Kwa hiyo kaza moyo, achana na dhambi zako.” (Revelation 3:19 Swahili)
“Nimekuwa nikiwapeni daima mfano kwamba kwa kufanya kazi mithili hiyo tunapaswa kuwasaidia walio dhaifu, tukikumbuka maneno ya Bwana Yesu mwenyewe: <Heri zaidi kutoa kuliko kupokea. »>” (Acts 20:35 Swahili)
“Yeye amhurumiaye maskini humkopesha Bwana,
naye atamtuza kwa aliyotenda.” (Proverbs 19:17 Swahili)
“Wapeni wengine wanavyohitaji, nanyi mtapewa. Naam, mtapokea mikononi mwenu kipimo kilichojaa, kikashindiliwa na kusukwasukwa hata kumwagika. Kwa maana kipimo kilekile mnachotumia kwa wengine ndicho ambacho Mungu atatumia kwenu. »” (Luke 6:38 Swahili)
“Lakini kila mmoja na aupime vizuri mwenendo wake mwenyewe. Ukiwa mwema, basi, anaweza kuona fahari juu ya alichofanya bila kuwa na sababu ya kujilinganisha na mtu mwingine.” (Galatians 6:4 Swahili)